Nomino ni majina ya watu, vitu, mahali, au wazo. Kuna aina nyingi za nomino k.v.
- Nomino za Kawaida
- Nomino za Pekee
- Nomino za Wingi
- Nomino za Dhahania
- Nomino za Vitenzi-Jina
- Nomino za Makundi
1) Nomino za Kawaida
Nomino za pekee ni maneno yanayorejelea vitu vya kawaida kama vile watu, nyumba, mahali, mimmea na vitu. Nomino za kawaida hazitumii herufi kubwa katikati ya sentensi kama nomino za pekee.
Mifano ya Nomino za Kawaida: Mkahawa, nyumba, mti, mwalimu, sahani, chupa, meli, mtoto, mwanafunzi, mtu, mji, mnyama, mbwa, ndege
2) Nomino za Pekee
Nomino za pekee ni majina spesheli yanayotumiwa kutambua nomino za kawaida kwa ubinafsi. Maneno yanayotaja majina mahususi ya watu, mahali, au vitu ambavyo vina sifa ya kipekee. Nomino za pekee hutumia herufi kubwa katikati ya sentensi.
Mifano ya nomino za pekee: Kemboi, Kisumu, Tom, Anna, Afrika, Ulaya, Nairobi, Kamau, Mlima Kenya, Tanzania, n.k.
3) Nomino za Wingi
Nomino za wingi ni nomino zinazorejelea vitu vinavyopatikana katika uwingi. Ni nomino ya vitu visivyohesabika.
Kwa mfano: Maji, mchanga, supu, chumvi, sukari, damu, wino, maziwa, mate, wali, mvua, unga, samli.
4) Nomino za Dhahania
Nomino za dhahania ni majina ya vitu visivyoweza kuonekana au kushikika kwa mkono. Ni maneno ya vitu vya kufikirika tu.
Mifano: Usingizi, shibe, furaha, huzuni, hekima, ubinafsi, uchoyo, maumivu, upendo, ukorofi, upole, ujinga, werevu, wema, kiu, elimu, ugonjwa.
5) Nomino za Makundi
Nomino za makundi ni nomino zinazohusika na vitu vinavyopatikana kwa makundi. Pia huitwa nomino za jamii.
Mifano ya nomino za makundi:
- Thureya ya nyota
- Halaiki ya watu
- Umati wa watu
- Mlolongo ya magari
- Fungu la maembe
- Baraza la wazee
- Shada la maua
- Chane ya ndizi
- Funda la maji
- Shehena ya mizigo
- Biwi la takataka
- Msafara wa magari
6) Nomino za vitenzi-jina
Nomino za vitenzi-jina ni nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi kwa kuongeza kiambishi “KU” mwanzoni mwa mzizi wa kitenzi.
Mifano: Kulea, kusoma, kulia, kucheka, kulima, kuandika, kutibu, kutesa, kuona, n.k.
Sentensi: Kucheka kwangu kumewaudhi wanaharakati wa mazingira.