How to Pass in KCPE Insha Paper

Example of KCPE Insha

Aina za Insha

Katika shule ya msingi, wanafunzi hufunzwa aina nyingi za insha:

 • Insha za methali
 • Insha za mjadala
 • Insha za Mdokezo
 • Insha za Mada
 • Insha ya mahojiano

Insha za Mjadala

Katika insha ya mjadala, mwanafunzi anatakiwa kutoa hoja za kuunga mkono au kupinga mada fulani. Kwa mfano:

Andika insha ya mjadala kuhusu mada: Serikali inapaswa kupiga marufuku uafiaji wa      mimba

Katika mfano huu, mwanafunzi anahitajika kutoa hoja kuunga mkono au kupinga sheria inayopiga marufuku uafiaji wa mimba. Mwanafunzi anaweza kutoa hoja za upande mmoja pekee utakaompa hoja za kutosha.

Insha za Kubuni

Katika shule ya msingi, insha za kubuni ni insha zinazompa mwanafunzi uhuru wa kubuni wahusika, maudhui na mazingira ya matukio fulani yasiyo halisi. Mifano ya insha za kubuni ni kama vile insha za methali, insha za mdokezo, insha za mada mahususi.

Kwa mfano: Andika insha juu ya mada Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.

Insha za Mdokezo

Insha za mdokezo ni insha za kubuni zinazoanzishwa au kumalizia kifungu fulani cha maneno. Mwanfunzi anapaswa kuendeleza kifungu kilichoanzishwa au kumalizia kifungu alichopewa.

Mfano wa insha ya kuanzishwa: Andika insha inayoanza na kifungu kifuatacho – Mama   aliniamsha asubuhi na mapema. Nikaoga, nikakunywa chai, kisha…

Katika insha kama hii, mwanafunzi anafaa asome kifungu kilichoanzishwa na aelewe vyema kabla kuiendeleza. Kisha, anatakiwa kufikiria kuhusu maudhui atakayozungumzia na kuipa insha yake mada inayofaa.

Insha ya Mada

Insha ya mada ni insha inayohusiana na mada maalum. Mwanafunzi anapaswa kutoa hoja au maelezo kuhusiana na mada aliyopewa. Insha nyingine ya mada huenda ikahitaji mwanafunzi atoe hadithi kuhusiana na mada fulani.

            Mfano 1: Andika insha juu ya mada “Umuhimu wa Miti”

Insha kama hii ni ya halisi na mwanafunzi hafai kuongezea chuku. Lengo ni kuonyesha kuwa mwanafunzi anajua kujieleza na kupanga hoja zake kwa njia mwafaka. Kwa mfano, mwanafunzi anatahiniwa kueleza maswala ibuka ya jamii kama vile kilimo, ukimwi, uchafuzi wa mazingira, ufisadi, na ukabila.

Mfano 2: Andika insha juu ya mada “Kisa cha Ajabu.”

Katika insha kama hii, mwanafunzi anaruhusiwa kueweka chuku katika maelezo yake. Anastahili kueleza matukio kwa mpangilio mzuri na lugha sahihi.

How to Pass Kiswahili Insha in KCPE

Ili kufaulu katika insha ya aina yoyote katika mtihani wa KCPE, mwanafunzi anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:

 • Kwanza, soma vizuri mada ya insha ili kuelewa barabara. Usipoelewa swali, utaenda kando na mada iliyokusudiwa na mtahini.
 • Pili, Andika insha kwa herufi kubwa na kuweka mstari. Usiandike nukta mwishoni mwa kichwa.
 • Ikiwa ni insha ya methali, ueleze maana ya methali katika aya ya kwanza, kisha uandike tukio au matukio yanayowiana na methali hiyo.
 • Hakikisha umeandika mwanzo (introduction) wa insha katika aya ya kwanza, itakayodokeza maswala utakayozingumzia katika insha.
 • Andika hoja moja katika kila aya. Usichanganye hoja zako. Kwa mfano, ukiambiwa uandike kuhusu umuhimu wa miti, unaweza kuandika hoja ya “mvuto wa mvua” katika aya ya pili. Usichanganye hoja ya “kuvuta maji” na hoja ya “kuzuia mmomonyoko wa udongo” katika aya moja.
 • Andika hitimisho katika aya ya mwisho itakayojumlisha hoja zako zote kwa ufupi.

Katika insha juu ya “Umuhimu wa Miti,” unaweza ukapanga hoja hivi:

 • Aya 1: Utangulizi (miti ni nini? Hupatikana wapi? Miti hufaa binadamu vipi? Umuhimu wa mada. Hoja kwa ufupi).
 • Aya 2: Miti huvutia/husababisha mvua
 • Aya 3: Miti huzuia mmomonyoko wa udongo
 • Aya 4: Miti hutoa chakula
 • Aya 5: Miti huleta hewa safi
 • Aya 6: Miti huleta mandhari mazuri
 • Aya 7: Hitimisho.

Examples of KCPE Insha Papers

Worst KCPE Insha Example

[tnc-pdf-viewer-iframe file=”https://kcsepdf.co.ke/wp-content/uploads/2020/07/Worst-Insha.pdf” width=”150%” height=”800″ download=”false” print=”false” fullscreen=”false” share=”true” zoom=”true” open=”true” pagenav=”true” logo=”true” find=”true” current_view=”true” rotate=”true” handtool=”true” doc_prop=”true” toggle_menu=”true” toggle_left=”true” scroll=”true” spread=”true” language=”en-US” page=”” default_zoom=”auto” pagemode=”none” iframe_title=””]

Average KCPE Insha Example

[tnc-pdf-viewer-iframe file=”https://kcsepdf.co.ke/wp-content/uploads/2020/07/Average-Insha-KCPE.pdf” width=”200%” height=”800″ download=”false” print=”false” fullscreen=”false” share=”true” zoom=”true” open=”true” pagenav=”true” logo=”true” find=”true” current_view=”true” rotate=”true” handtool=”true” doc_prop=”true” toggle_menu=”true” toggle_left=”true” scroll=”true” spread=”true” language=”en-US” page=”” default_zoom=”auto” pagemode=”none” iframe_title=””]

Best KCPE Insha Example

[tnc-pdf-viewer-iframe file=”https://kcsepdf.co.ke/wp-content/uploads/2020/07/Best-Insha.pdf” width=”200%” height=”1000″ download=”false” print=”false” fullscreen=”false” share=”true” zoom=”true” open=”true” pagenav=”true” logo=”true” find=”true” current_view=”true” rotate=”true” handtool=”true” doc_prop=”true” toggle_menu=”true” toggle_left=”true” scroll=”true” spread=”true” language=”en-US” page=”” default_zoom=”auto” pagemode=”none” iframe_title=””]

(Visited 3,528 times, 1 visits today)

KCSEPDF.CO.KE

kcsepdf.co.ke is an online learning platform where tutors and students can access notes, revision questions, educative articles, stories, e-books, and more learning materials.

3 thoughts on “How to Pass in KCPE Insha Paper

Leave a Reply

Kiswahili Notes and Past Papers

Mambo ya kuzingatia unapoandika insha

Kuna baadhi ya mambo au masharti ya kuzingatia ili uandike insha bora. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi Mpangilio mzuri wa hoja – kila aya lazima iwe na hoja maalum iliyoelezwa kwa upana na ufasaha. Urefu wa kutosha wa insha – sana sana ukurusa moja na nusu had kurasa mbili. Lugha sanifu isiyokuwa na makossa ya […]

Read More
Kiswahili Notes and Past Papers

Aina za Nomino

Nomino ni majina ya watu, vitu, mahali, au wazo. Kuna aina nyingi za nomino k.v. Nomino za Kawaida Nomino za Pekee Nomino za Wingi Nomino za Dhahania Nomino za Vitenzi-Jina Nomino za Makundi 1) Nomino za Kawaida Nomino za pekee ni maneno yanayorejelea vitu vya kawaida kama vile watu, nyumba, mahali, mimmea na vitu. Nomino […]

Read More
Kiswahili Notes and Past Papers Revision Notes and Questions

Kiswahili KCSE Past Papers

Hello, you can download free KCSE question papers for Kiswahili here. Access past KCSE question papers and free KCSE revision papers; free download PDF. KCSE-2011-KISWAHILI-PAPER-1 KCSE 2011-KISWAHILI-PAPER-2 KCSE-2011-KISWAHILI-PAPER-3 KCSE-2012-KISWAHILI-P1 KCSE-2012-KISWAHILI-P2 KCSE-2012-KISWAHILI-P3 kiswahili-paper-1-form-3-term-1-exam-2018 kiswahili-paper-1-term-2-exam-2018 kiswahili-paper-2-form-3-term-1-exam-2018 kiswahili-paper-2-term-2-exam-2018 kiswahili-paper-3-term-2-exam-2018

Read More