Maswali ya Tumbo Lisiloshiba

High school revision questions
  1. Alifa chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine

“Doa ndio kawaida inayobainisha maisha ya mwanadamu.”Onyesha ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa hadithi za: Shogake Dada ana Ndevu, Mame Bakari, Shibe Inatumaliza na Mtihani wa Maisha. (alama 20)

2. Na kwa nini hazitaki kuukemea mfumo huu wa maisha? Mfumo wa mwenye nacho kuendelea kupata na msinacho kuendelea kukosa?

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

b) Fafanua maudhui mawili yanayodhihirika katika dondoo hili (alama 4)

c) Tambua na ueleze sifa sita za msemaji (alama 6)

d) Eleza athari ya “ msinacho kuendelea kukosa” katika jamii husika (alama 6)

3. Fafanua jinsi suala la elimu limeshughulikiwa katika Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine kwa kurejelea hadidhi zifuatazo:

a) Mapenzi ya Kifaurongo (alama 5)

b) Shogake Dada ana Ndevu (alama 5)

c) Mtihani wa Maisha (alama 5)

d) Mwalimu Mstaafu (alama5)

4. “… Basi niache nitafute pesa. Muhimu mniunge mkono…”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

(b) Fafanua sifa zozote nne za mzungumziwa (alama 4)

(c) Fafanua athari ya vitendo vya mzungumzaji wa maneno haya katika jamii (alama 12)

Jadili suala la uozo wa maadili katika jamii huku ukirejelea hadithi zozote nne katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (alama 20)

5. Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukerejelea hadithi fupi zifuatazo.

a) Mapenzi ya kifa urongo (alama 5)

b) Shogake Dada ana Devu (alama 5)

c) Mame Bakari (alama10)

6. Ndoto ya mashaka: Ali Abdalla Ali

“Sasa nimechoka mja. Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi. Hadilini haya mashaka ya kutengenezwa? Mashaka ya mashaka!”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

b) Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika (alama 4)

c) Fafanua mambo sita yanayomfanya mrejelewa aradue kufa. (alama12)

7. “Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)

b) Tambua tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili

c) Fafanua sifa nne za msemaji (al 4)

d) Jadili maudhui ya utabaka ukirejerea hadithi husika (al 10)

8. Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi;

a) Mapenzi ya kifaraurongo (al 10)

b) Mame Bakari (al 10)

9. “Madhila ya mtoto mvulana katika karne ya ishirini na moja ni mengi.” Tetea kauli hii kwa hoja ishirini ukirejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Masharti ya Kisasa na Ndoto ya Mashaka. (alama 20)

10. Salma Omar: Shibe Inatumaliza

(a) “Sijali lawama mnonilaumu”

(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(ii) DJ na wenzake wanaonekana kufurahia maudhui ya wimbo huu. Thibitisha. (alama 6)

11. Alifa Chokocho: Shogake Dada ana Ndevu

“…tumshukuru kwa jinsi alivyomwongoza na kumwelekeza kwenye njia iliyonyooka” Ukirejelea wasifu wa Safia, tetea na upinge kauli hii. (alama 10)

12. Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo, onyesha jinsi jamii imegawanyika kitabaka kuegemea.

i. Kielimu

ii. Kikazi

iii. Kiuchumi (alama 20)

13. SHIBE INATUMALIZA

“Ndugu yangu kula kunatumaliza” “Kunatumaliza au tunakumaliza”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)

b) Fafanua maana kitamathali katika kauli ‘Kula tunakumaliza’ (al. 10)

c) Kwa mujibu wa hadithi hii, kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza? (al.6)

14. ‘MAME BAKARI’

Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake, onyesha kwa mifano mwafaka. (al. 10)

15. ‘MASHARTI YA KISASA’

“…………… mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.”

Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (al. 10)

16. Jadili jazanda za anwani katika hadithi zifuatazo

a) Shibe Inatumaliza (alama8)

b) Mtihani wa maisha (alama6)

c) Mkubwa

17. MAPENZI YA KIFAURONGO

a) “Kutazama shule za vijijini kumwibua bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.”

b) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

c) Tambua mbinu moja ya lugha kwenye dondoo hili. (alama 2)

d) Jadili maudhui yafuatayo katika hadithi hii

i) Mabadiliko (alama 5)

ii) Uozo (alama 5)

18. “… maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili. (alama 4)

c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana? (alama 6)

d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili. (alama 6)

19. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi. (alama 20)

20. “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)

c) Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili. (alama 10

21. “Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”

i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii. (a 8)

22. Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”(alama 8)

23. Sekta ya elimu ina changamoto nyingi. Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo: (alama 20)

a) Mapenzi ya Kifaurongo

b) Shogake dada ana Ndevu

c) Mwalimu Mstaafu

d) Mtihani wa maisha

24 ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’

i) Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya

Tumbo Lisiloshiba (al 10)

ii) Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi. (al 10)

25. “Mame Bakari” (Mohamed Khelef Ghassany)

“Dunia we’ dunia. Dunia ya mwenye nguvu, si ya mimi dhaifu wa nguvu. Dunia ya msumari moto juu ya donda bichi.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)

(b) Ni mbinu ipi iliyotumika katika dondoo hili? (alama 2)

(c) Taja baadhi ya maamuzi ya maana yaliyofanywa na msemaji wa dondoo. (alama 6)

“Tulipokutana Tena” (Alifa Chokocho)

“Hivi ndivyo maisha yapasavyo kuwa-huru kabisa.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Ukirejelea hadithi, thibitisha kuwa mmoja wa wahusika hawa hakuishi maisha ya awali inavyopasa. (alama 16)

26. Fafanua maudhui ya umaskini yanavyojitokeza katika hadithi Tumbo Lisiloshiba na Tulipokutana Tena. Zingatia hoja nne nne kwa kila hadithi. (alama 20)

27. “Shogake Dada ana Ndevu” (Alifa Chokocho)

“Halindwi, hujilinda yeye mwenyewe. Hujilinda ndani sikwambii nje.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Onesha tamathali mbili za usemi kwenye dondoo. (alama 2)

(c) Fafanua sifa saba za anayerejelewa katika kauli hii. (alama 14)

28. Kwa kurejelea hadithi zozote tatu katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine, jadili vile waandishi walivyoshughulikia suala la mapuuza katika jamii. (alama 20)

29. “Mtihani wa Maisha” (Eunice Kimaliro)

“ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Fafanua sifa sita za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)

(c) Taja mambo mbalimbali yanayochangia adhabu ya mrejelewa wa dondoo hili. (alama 10)

30. Kwa kurejelea hadithi zozote tatu katika Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine, onesha vile waandishi walivyotumia mbinu ya taswira. (alama 20)

31. “Kauli yake ni kama maji ya moto yasiyoweza kuchoma nyumba.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)

b) Taja na ueleze umuhimu wa tamathali moja ya usemi iliyotumika katika dondoo. (Alama 2)

c) Fafanua sifa za wapuuzaji wa kauli iliyotolewa. (Alama 8)

d) Jadili dhima sita za mrejelewa katika dondoo. (Alama 6)

(Visited 7,503 times, 1 visits today)

KCSEPDF.CO.KE

kcsepdf.co.ke is an online learning platform where tutors and students can access notes, revision questions, educative articles, stories, e-books, and more learning materials.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KCSE Past Papers

Diet Therapy KNEC Past Papers

Download free Diet Therapy, Accounting and Control KNEC Notes and Past Papers – Diploma in Catering and Accommodation Management KNEC Past Papers Diet Therapy, Accounting and Control 2017july

Read More
KCSE Past Papers

Applied Geometry KNEC Past Papers – Artisan

Download free KNEC Notes and Past Papers on Applied Geometry KNEC Past Papers Applied Geometry 2018n Applied Geometry 2021j

Read More
KCSE Past Papers

Physical Science KNEC Past Papers

Download KNEC past exam papers for Physical Science, Mechanical Science, and Electrical Engineering Physical Science KNEC Past Papers March 2015 Diploma in Electrical Engineering Murang’a University Physical Science, Mechanical Science and Electrical Engineering Principles – KNEC Past exam Papers – Jul 2015 Physical Science, Mechanical Science and Electrical Engineering Principles – KNEC Past exam Papers […]

Read More